Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Nyakaji Etanga amempokea Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya siku ya Alhamis tarehe 24/06/2025.
Mhandisi peter amefika Wilayani Kilolo, kwa ajili ya kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Slaa kuhusiana na changamoto za kimtandao wanazopata wananchi wa kata ya Irole kijiji cha Ibofwee, na pia kuanzisha maabara ya kompyuta katika shule ya Sekondari Nyalumbu.
Bi. Nyakaji amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano kufika ili kuyanyia kazi yale yote aliyoelekezwa na kumuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha ili lengo lifikiwe na wananchi wazidi kufurahia huduma zinazotolewa na Serikali yao kwa maendeleo ya Wilaya ya Kilolo.
Mhandisi peter, aliongozana na Mkurugenzi kufika katika maeneo hayo mawili ili kujionea aweze kuyafanyia kazi ukaribu zaidi, ambapo katika shule ya Sekondari Nyalumbu ameahidi kufanikisha na kuiwezesha maabara ya kopyuta mpya ikiwa na vifaa vyake vyote kukamilishwa ndani ya mda mchache. Huku kwa upande wa changamoto za mawasiliano katika kijiji cha Ibofwee, atawasiliana na wahusika kwa haraka ili waje waweke kambi hapo kushughulikia changamoto hio na wananchi waanze kufurahia huduma kwa wakati na mahali popote watakapokuepo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Ellah Msigwa amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano kwa wote, na kumuomba utekelezaji uanze mapema ili kuharakisha maendeleo na huduma kwa wananchi, kwani mawasiliano kwa sasa ndio gurudumu la kila mtu kuyafikia maendeleo katika jamii.
Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ulianzishwa kwa lengo kubwa la kupeleka na kufanikisha huduma ya mawasiliano kwa Wananchi waishio katika maeneo machache ya mjini na maeneo mengi yaliyo mbali vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa