\Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ndugu Hassan Mnyikah ametoa rai kwa Wasimamizi wa lishe Wilaya, wajitoe kwa nguvu zote na wasimamie vizuri miradi yote ya lishe ili jamii ipate kunufaika, na wapatiwa elimu ya kutosha ili wawe na uelewa mzuri na kuona umuhimu wa kuwa na tabia ya kula mlo kamili wenye virutubisho vitakavyopelekea kuwa na jamii/kizazi chenye nguvu, ufikiri mzuri na imara.
“hakikisheni mnaratibu vizuri elimu ya lishe kuanzia ngazi ya Kitongoji, Kijiji hadi Katani ili wanachi wapate kujua umuhimu na faida za kula vyakula vyenye virutubisho ili waepukane na maradhi.” Alisema Mnyikah
Aidha kwa upande wake mratibu wa lishe wilaya Bi. Bertha Mwakabage amesisitiza jamii ipewe elimu endelevu kuhusiana na lishe lakini jitihada za maksudi zielekezwe kwa wajawazito kushauriwa kufika kliniki mapema zaidi ili wapatiwe elimu nzuri kuhusiana na aina ya vyakula vyenye virutubisho ili kumwezesha mama na mtoto atakayezaliwa kuwa na afya njema.
“watoto wengi wanaozaliwa sasahivi wanakuwa na changamoto mbalimbali za kiafya na hii inasababishwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa baadhi ya madini mwilini kutokana na akina mama wengi kutokufika kliniki kwa wakati ili washauriwe aina ya vyakula wanavyopaswa kula.”
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa