Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Anna Msola imetoa pongezi kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ndugu Hassan Mnyikah na timu yake ya Wataalamu kwa kuweza kukusanya kiasi cha Tshs 576,965,523/- kwa mwezi wa kumi tu ambacho ni zaidi ya kilichokusanywa mwezi wa tisa.
Anna Msola ametoa pongezi hizo tarehe 21/11/2024 wakati akiongoza kikao cha kawaida cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Aidha kwa upande mwingine Mhe. Anna Msola aliweka msitizo kuhusiana na swala zima la upungufu wa madawati na viti na kumtaka Mkurugenzi kuhakikisha anakua na mikakati madhubuti ya kufanikisha upatikanaji wa madawati kabla ya Januari ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza watapokelewa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Ndugu Hassan Mnyikah ameyapokea maelekezo ya kamati na kuahidi kuyatekeleza kwa wakati na ifikapo mwezi wa kwanza, upungufu wa madawati kwenye shule zote utakua umekwisha.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa