Timu ya ukaguzi kutoka mkoani imefanya ziara ya siku tatu katika halmashauri ya wilaya ya kilolo kwa kutembelea na kukagua miradi yote ya maendeleo inayoendelea na ujenzi. Lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inakamilishwa kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, ili wananchi waweze kunufaika na huduma zitakazotolewa pindi miradi ikikamilika.
Wakizungumza baada ya kuhitimisha zoezi hilo, walitoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na halmashauri kwenye miradi yote waliyopitia huku wakishauri changamoto ndogondogo walizobaini wazifanyie kazi kwa haraka ili miradi yote ikamilishwe ifikapo Januari.
Aidha kwa upande wa halmashauri wameishukuru timu hiyo kwa kufika kilolo na kuahidi wameyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati ili miradi yote ikamilike ndani ya mda. Ziara hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 10-12-2024 hadi 13-12-2024.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa