• Kero |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Kilolo District Council
Kilolo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo,Umwagiliaji na ushirika
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi,Maliasili na Mazingira
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu
      • Ufugaji
    • Afya
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Customers services agreement
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofis au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

MBOLEA YA RUZUKU IWAFIKIE WAKULIMA KATANI - DIWAN, IDETE

Posted on: November 8th, 2024

Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kimefanyika leo tarehe 8-11-2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Kilolo chini ya mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Anna Msola,  kwa lengo la kujadili taarifa za utekelezaji za robo ya kwanza (Julai – Septemba) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Akiwasilisha taarifa ya kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Rahman Mkakatu,iliibuliwa hoja ya mbolea ya ruzuku kwa wakulima na Mhe. Bruno Kauku kuhusiana na upungufu wa mbolea katika kata yake.

“ Mhe. Mwenyekiti wakazi wa kata ya Idete wanalazimika kufuata mbolea ya ruzuku Bomalang’ombe kutokana na wafanyabiashara/mawakala kushindwa kupeleka Idete kutokana na gharama kua juu za usafirishaji, je Serikali ina mpango gani wa kulitatua hilo?” aliuliza Mhe. Kauku.

Aidha Mhe.Bruno Kauku ameiomba Serikali kufanya jitihada za kuwahisha kupeleka mbolea kwa wakulima wa kata hiyo kwani wao wanawahi kuanza msimu mpya wa kilimo ukitofautisha na maeneo mengine, hivyo kukosa mbolea hiyo kwa wakati itarudisha nyuma shughuli za kilimo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Mhe. Anna Msola amemuagiza Afisa kilimo wa wilaya hiyo kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu ili wakulima wote wenye uhitaji wa mbolea waweze kujiorodhesha ili uhitaji ujulikane na kisha wapelekewe kwa wakati ili kufanikisha uzalishaji wa mazao kwa tija zaidi.

Wakati huohuo baadhi ya waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali wameunga mkono hoja hiyo kwa kueleza kwamba tatizo la kutopatikana kwa mbolea katika baadhi ya maeneo huwakatisha tamaa wakulima na kushindwa kuendelea kulima kutokana nakushindwa kugharamia gharama za kuzifuata mbolea hizo maeneo ya mjini na kwingineko, hivyo wanapendekeza serikali ione ni jinsi gani mbolea za ruzuku zitawafikia wakulima katika kila  kata kwa bei elekezi ya serikali.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo,Dkt. John Mwingira ameeleza kwamba amelipokea ombi hilo kutoka kwa wakulima kupitia kwa madiwani hivyo inachotakiwa ni wakulima kujiorodhesha kwa majina kwa wale wanaohitaji mbolea hizo ili serikali iweze kuona ni kwa utaratibu upi mbolea hiyo itawafikia.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA WATUMISHI WA UMMA December 23, 2024
  • Waliochaguliwa kuhudhuria usaili wa "Oral" October 10, 2024
  • Kuitwa usaili wakusanya mapato October 16, 2024
  • KUITWA KAZINI October 29, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MWENGE WA UHURU 2025 WARIDHIA MIRADI YOTE KILOLO DC

    April 30, 2025
  • WILAYA YA KILOLO KUFANYA MAONYESHO MAKUBWA YA BIASHARA, KILIMO NA VIWANDA

    April 16, 2025
  • MAFUNZO ELEKEZI KWA AJILI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI.

    January 14, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI (WASIMAMIZI) NGAZI YA JIMBO KILOLO YATAMATIKA

    December 20, 2024
  • Angalia zote

Video

Jinsi ya Kupata leseni ya Biashara kupitia simu ya Mkononi
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Tangazo la Ajira

Viungio vinavyohusiana

  • Public Service Management
  • Watumishi Portal
  • PO-RALG
  • National Examination Council
  • eGA
  • Mkoa wa Iringa
  • Mufindi DC
  • Iringa DC
  • Iringa MC

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya

    Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo

    Simu ya mezani: 0262968010

    Mobile:

    Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa