Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kilolo(KUU), imetembelea na kufanya ukaguzi wa Miradi ili kujionea jinsi inavyotekelezwa na kusimamiwa ili wapate kujiridhisha kama inafwata ubora na itakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.
Ziara hiyo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Mhe. Estomin Kyando ambaye aliongozana na katibu tawala wilaya, ametoa maelekezo kw wahandisi wa halmashauri wawe wanafika na kushinda site ( kwenye miradi) kila siku ili waweze kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
“Wahandisi acheni kujifungia ofisini tuu, tokeni muende site ambapo miradi inatekelezwa ili muwasimamie mafundi kwa ukaribu na muwaelekeze vizuri ili miradi yetu ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaokidhi viwango, ili wananchi waweze kufurahia huduma.” Amesema kyando
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na shule mpya za Msingi na Sekondari ambazo ni Msombwe na kipaduka zilizopo kata ya Uhambingeto.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Kemilembe Kafanabo ameishukuru KUU Wilaya kwa kutembelea miradi hiyo na kuwahakikishia kuwa yale yote walioshauri na kuagiza watayafanyia kazi kwa ukaribu zaidi ili lengo linalokusudiwa liweze kufikiwa kwa wakati kwa maslahi mapana ya halmashauri yetu.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ilifanya ziara hiyo tare 10 – 11/07/2025.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa