UTANGULIZI
Wilaya ya Kilolo ilianzishwa rasmi Januari 2006, baada ya kugawanyika Wilaya ya Iringa.Ina eneo lenye ukubwa wa sq.km 7,881.Wilaya inapakana na Wilaya ya Mpwapwa kwa upande wa Kaskazini,kwa upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na Wilaya ya Kilosa,Wilaya ya Kilombero kwa upande wa Mashariki,Wilaya ya Mufindi kwa upande wa Kusini na Wilaya ya Iringa kwa upande wa Magharibi.
Kiutawala, Wilaya ina Tarafa 3,Kata 22,Vijiji 106 na Vitongoji 555.Ina jumla ya wakazi 225,589 kati yao 113,117 ni wanawake na 112,475 ni wanaume .Makabila makuu ni Wahehe na Wabena na wengine ni Wakinga na Wasagara.Shughuli kuu za kiuchumi ni Kilimo na Ufugaji. Wilaya ina Baioanuai adimu na zisizo adimu katika Maeneo ya Misitu ya hifadhi ya Kilombero-Magharibi,Uzungwa Scarp,Image,Kising’a-Lugalo,Kawemba,Kilanzi-Kitunguru,Kitemele na Kitonga-Kihulula,yenye jumla ya Ha.225,006.Misitu hiyo imepakana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa na Pori la Akiba la Chita
FURSA ZA UTALII NDANI YA WILAYA
Wilaya ya Kilolo ina utajiri mkubwa wa asili na utajiri wa kiutamaduni,ambao ni Mapango ya asili,Maeneo ya Kihistoria,Miamba ya asili,Mabwawa ya asili,Wanyamapori na ndege adimu na wasio adimu kupatikana duniani,Mandhari ya Maumbile ya asili ambayo ni Misitu,Milima,Mito na Maporomoko ya maji.Kazi za mikono za asili hususan uchoraji,ususi, na ufinyanzi,pamoja na Mila na desturi za kabila la Wahehe. Aina za Utalii unaowezekana katika Maeneo yaliyotajwa ni Utalii wa Picha,Utalii wa Kihistoria,Utalii wa Ki-ikolojia,Utalii wa Utamaduni,Utalii wa kupanda Milima,Utalii wa Ndege,Utalii wa Wanyamapori na Utalii wa Utafiti.Mchanganuo wa Vivutio vya Utalii ni:
Anapatikana katika msitu uliohifadhiwa wa Kilombero Magharibi wenye baioanuai nyingi za mimea,wanyama na ndege adimu na wasio adimu. Wanyama wengine wanaopatikana ni pamoja na Mbega weupe na weusi na Mbega wekundu.Hifadhi hii inapatika kijiji cha Udekwa km 143 kutoka makao makuu ya halishauri na baraba zake inapitika mwaka mzima
2.Mapango ya Asili ya Magombelema
Mapango ya asili yenye vyumba vya kupumzikia 8
-Eneo linatumiwa na wakazi kwa ibada za asili/Matambiko
-Kuna popo wenye meno
-Chifu Mkwawa pamoja na askari wake walitumia eneo hili kama maficho dhidi ya adui.
-Yamezungukwa na Msitu uliohifadhiwa wa Kilombero wenye Baioanuwai nyingi za wanyama,mimea na ndege wa aina mbalimbali.Inapatikana kijiji cha udekwa km143 kutoka makao makuu ya halmashauri,barabara zake zinapitika mwaka mzima
3.Kaburi la NyundoKaburi
-Ni kivutio cha Utalii unapoweza kupata kumbukumbu za kihistoria
-walipozikwa askari 300 wa Kijerumani baada ya kuuwawa na askari wa Mkwawa mwaka 1898 katika vita kati ya Wajerumani na Wahehe
4.Mwamba au Jiwe la Asili liitwalo Liganga la mtwivila
-Eneo linalotumiwa na wakazi kwa ibada za asili/Matambiko
-Majani yaotayo juu ya jiwe yajulikanayo kwa lugha ya Kihehe kama Mafwelefwenzi au
-Syzigium specie kisayansi hutumika kutibu maradhi ya asthma na kikohozi.
-Ni jiwe lenye ukubwa wa ekari 12
5.Maporomoko ya maji ya Kifung’a
-Ni Maporomoko yenye urefu wa mita 8 kwenda juu.
- baadhi ya viumbe hai kama samaki wanapatikana
-yanapatika Magome km 63 kutoka Kilolo
6.Eneo Oevu/Bwawa la asili la Nyautwa (Nyautwa spiritual swamp)
Maji ya bwawa hili huchanganywa na majani yaotayo ndani ya bwawa kutibu maradhi mbalimbali kama vile Kifafa,
ukoma na kutibu mtu aliyerukwa na akili.
Maji hayatumiwi kwa shughuli nyingine kama kuoga, kufua, kunywa na kupikia.
-Inapatikana Masege km 47 kutoka Kilolo na barabara inapitika kwa mwaka mzima
-Ni mazalia na makazi ya ndege maji.
-Inafaa kwa uwekezaji wa kitalii (camping)
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa