a.Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuendesha biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu bila ya kuwa na leseni ya usafirishaji
b.Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu atatakiwa kupeleka maombi ya leseni kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zinajumuisha Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilayaā€¯
c.Pikipiki za magurudumu mawili na matatu zinatoa huduma za usafiri wa abiria zitakuwa na vibao vyenye namba ya usajili vilivyoandikwa kwa maandishi meusi na vibao vyeupe
d.Leseni zitatolewa tu kwa muombaji ambaye ni mwanachama wa umoja uliosajiliwa
e.Mtu ambaye atafanya biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili au matatu bila ya kuwa na leseni ya usafirshaji atakuwa amevunja Sheria ambapo atashitakiwa na kutozwa faini kati y ash 50,000 hadi 100,000 au kufungwa jela kati ya miezi 6 na mwaka mmoja.
Kuwasilisha maombi ya leseni
Leseni za usafirishaji wa abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu zitatolewa na Afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi wa Jiji/Mji/Wilaya au Manispaa husika ambaye atajulikana kama Afisa Mteule. Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Afisa aliyeuliwa kwaajili ya Kutoa leseni za usafirishaji wa abiria kwa pikipiki ni Afisa Biashara wa Wilaya.
Muombaji wa Leseni za usafirishaji abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu atajaza fomu ya maombi akiambatisha viambatisho vifuatavyo:
a) Nakala ya kadi ya uanachama na barua ya utambulisho kutoka katika Umoja/Chama/Ushirika uliosajiliwa rasmi na Serikali;
b) Nakala ya Cheti halisi cha usajili wa pikipiki ya magurudumu mawili au matatu;
c) Nakala ya Bima ya pikipiki kwa ajili ya abiria watakaopanda pikipiki husika;
d) Taarifa ya ukaguzi kutoka kwa mkaguzi wa vyombo vya moto (V.I.R);
e) Ikiwa ni Kampuni, Umoja au Chama, awasilishe cheti cha usajili wa umoja au chama au Kampuni;
f) Nakala ya leseni ya kuendesha pikipiki pamoja na picha za dereva za hivi karibuni;
g) Nakala ya mkataba wa ajira kati ya dereva na mmiliki wa pikipiki husika,
h) Nyaraka zozote za ziada zinazoweza kuhitajika na SUMATRA.
Baada ya Afisa Mteule wa Wilaya kupokea fomu ya maombi ya leseni pamoja na viambatisho vyake atakagua kwa lengo la kujiridhisha kuwa taarifa zilizopo ni sahihi na akiridhika na yaliyomo kwenye fomu ya maombi ya leseni pamoja na viambatisho, kabla ya kutoa leseni atamuelekeza muombaji kulipa ada ya leseni:
Pia atalipia Kila fomu ya maombi Tshs: 2,000/=
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa