Dr. mrutu alisema mradi upo katika mikoa nane(8) na shule 91 katika mikoa hiyo ambapo mradi unatoa vitabu na vifaa vya michezo ambapo kila shule ilikabidhiwa vitabu 310 vikiwemo vitabu vya lugha ya Kiswahili na kiingereza,vitabu vya kiada 82 na vifaa vya michezo 41 vitabu hivi vimethibitishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania(TIE).Shule hizo ni Kitowo,Mwatasi,Mwanzala,Luganga na Kilolo B kwa upande wa iringa ni Kitayawa,Mangalali,Isakalilo,Ilambilole na nyang'oro
Dr. Mrutu aliongeza kuwa lengo la mradi huu ni kuchochea tabia ya wanafunzi kupenda na kujenga tabia ya kusoma vitabu ili kupata maarifa mbali mbali yatakayowawezesha kutatua changamoto za maisha na kutumia vifaa vya michezo walivyopewa ili kuimarisha utimamu wa miili yao kwa kushiriki michezo.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa