Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Elimu ya Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mhe. Sadath Mfugwa akipokea taarifa za maendeleo ya miradi ya Elimu na Afya kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025 (Julai mpaka Septemba) amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta vifaa vya kisasa katika hospital ya Wilaya.
Katika kikao hicho Wajumbe wa Kamati walipata nafasi ya kusikiliza,kuchangia, kukosoa na kushauri mambo mbalimbali katika Afya na Elimu kwa lengo la kujenga na kuboresha.
“tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea vifaa vya kisasa katika hospitali yetu ya Wilaya ya Kilolo kama vile Mtambo wa X-ray (digital X-ray machine) na uwezeshwaji wa duka kubwa la serikali la kuuza dawa.”
Aidha Mhe. Sadath alitoa rai kwa wataalamu wa Manunuzi kuhakikisha wanapotangaza tenda, wanapatikana wazabuni zaidi ya mmoja ili waweze kusambaza vifaa vya ujenzi kwa ufanisi katika maeneo ya kazi ili miradi ya Elimu na Afya ikamilike kwa wakati na wananchi wanufaike.
Wajumbe wa kamati kwa upande wao walisisitiza Elimu ya watu wazima ipewe kipaumbele ili kutatua tatizo la watu kutojua kusoma na kuandika na hivyo kushauri jitihada za makusudi zichukuliwe kukabiliana na changamoto hio.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa