Jukwaa hilo lilizinduliwa rasmi tarehe 17/05/2017 na Mh.Asia Juma Abdalah mkuu wa Wilaya ya Kilolo.Lengo la kuanzisha jukwaa la Uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ni kukutana na kujadiliana fursa,changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za kiuchumi.Vilevile kuongeza uelewa wa wanawake katika uchumi,biashara,upatikanaji wa mtaji,sheria za nchi katika masuala ya uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi.
Wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi hapa Tanzania na duniani kote. Hii inatokana na kutokuwa na usawa katika Fursa, uwezo wa kupata mitaji, ajira na baadhi ya maeneo malipo ya kazi kwa wanawake yamekuwa sio sawa na wanaume. Kuondoa matabaka na sheria ambazo zitasaidia kuondoa ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake ni jambo la muhimu sana kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na familia. Ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi ni kichocheo kizuri cha maendeleo ya nchi yetu na jamii kwa ujumla.
Katika kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo pia yamesisitiza uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa aliteua timu ya viongozi na wataalam ambao wanafanya kazi kama chombo cha juu katika kutambua na kuweka mikakati ya kupunguza na kuondoa pengo kubwa ambalo limejengeka duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani kote.
Timu hii inaangalia mambo muhimu ambayo yatasaidia kurekebisha hali iliyopo sasa. Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kwa kuhakikisha Malengo ya Maendeleo endelevu yanafikiwa na malengo ya 50/50 ya dunia kufikiwa mwaka 2030.
Katika timu iliyoteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Mh. Makamu wa Rais mama Samia Hassan Suluhu ni mjumbe, hivyo Mh. Makamu wa Rais ameelekeza kuwepo na Majukwaa ya Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi katika Mikoa yote na Halmashauri zote za Tanzania. Majukwaa haya yatasaidia kuongeza uelewa wa wanawake katika Uchumi, biashara, upatikanaji wa mitaji, sheria za nchi katika masuala ya Uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni chombo ambacho kilianzishwa ili kuratibu na kuongoza shughuli zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinazoendeshwa na Sekta ya Umma na Binafsi. Baraza pia linasimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuwaongoza watanzania kwenye uchumi imara na kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara na uchumi shirikishi yanakuwepo.Aidha Mh.Bi Asia Abdalah alisisitiza wajumbe wote ambao wako kwenye hilo jukwaa "ni wajibu wetu sasa sisi ambao tuko kwenye chombo hiki kuhakikisha miongozo,maelekezo na taratibu zote ambazo tunapewa na wataalamu wetu tunazifanya nukta kwa nukta neno kwa neno mstari kwa mstari na hivyo ndivyo ambayo tunaweza kubadilisha maisha".Pia mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Valence Kihwaga aliwataka waratibu wa majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi ngazi ya kata yakafanye kazi kushirikiana na wananchi ili jukwaa hili litakapo kutana kwa mara ya pili kufanya tathimini yale yaliyopendekezwa kwenye uzinduzi wa jukwaa yawe yamefanyiwa kazi kwa lengo la kuleta mabadiliko
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa