Mh.Jafo Suleiman Said amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Kilolo kufuatia maagizo aliyoyatoa alipotembelea wilaya hii mwaka jana September.Hospitali hiyo inategemea kukamilika ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu.Lengo kuu la ujenzi wa hospitali ni kusogeza huduma za Afya karibu na jamii ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Afya ya mwaka 2009 na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama Tawala ya mwaka 2015. Mradi huu umelenga kuhudumia wakazi wanaokadiriwa kuwa 229,146 kutokana na kasi ya ukuaji wa watu unaokadiriwa kuwa 1.7% kwa mwaka kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 .Mradi huu unasimamiwa na wakala wa Majengo Tanzania(TBA)ambao wameingia memoranda ya makubaliano na Halmashauri katika kutekeleza jukumu hili muhimu kwa lengo la kuhakikisha kazi inayofanyika inaendana na thamani ya fedha iliyotumika. Aidha Mh.Jafo Suleiman alisisitiza halmashauri kwa upande wake ifanye ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa uadilifu mkubwa ili miradi yote iliyoanzishwa iweze kukamilika kwa wakati na katika viwango vinavyokubalika.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa