Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Wilayani Kilolo umezindua jumla ya miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya 14,923,909,000 (Bilioni kumi na nne milioni miatisa ishirini na tatu mia tisa na tisa elfu tu) Miradi hiyo Kisekta ni miradi ya Utawala mmoja, Elimu mmoja, Ujenzi mmoja, afya mmoja, Biashara na viwanda mmoja, Maendeleo ya Jamii mmoja, Kilimo mmoja na TAKUKURU mmoja.Miradi iliyotembelewa na mwenge wa Uhuru ni Ujenzi wa Ofisi ya kijiji Kitelewasi,Ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Lundamatwe,klabu ya kupambana na rushwa shule ya sekondari Lundamatwe,ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mji mdogo wa Ilula,Ujenzi wa zahanati katika kijiji cha kipaduka,Ujenzi wa kiwanda cha nyanya Ikokokoto,Mradi wa kikundi cha kufuga samaki na Ujenzi wa mradi wa skimu ya umwagiliaji mgambalenga katika kijiji cha Mtandika.
Miradi hiyo imefunguliwa na Mkimbiza mwenge kitaifa ndugu Amor Hamad Amour ambapo alisisitiza halmashauri kusimamia kwa karibu miradi yote kwa lengo la kuhakikisha inakamilika kwa muda uliopangwa ili wanaichi waweze kuifaidi pia amewaasa wanainchi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu jinsi miradi hiyo inavyotekelezwa ili baadaye waweze kuitunza vizuri.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa