Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mhe. Rahman Mkakata, ameongoza kikao cha Kamati hiyo leo tarehe 30-10-2024 katika ukumbi wa Halmashauri kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo zinazotekelezwa katika kipindi cha Robo ya Kwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilicho anza Julai hadi Septemba 2024.
Mhe. Rahman alihoji tabia ya watu wanaochoma misitu/mapori kwa nadharia wanasafisha mashamba na kupelekea kusababisha uharibifu mkubwa kutokuchukuliwa hatua za haraka ili kukomesha tabia hiyo ovu.
“kuna watu wao kazi yao ni kuanzisha moto katika mapori/misitu na kufanya uharibifu mkubwa unaoleta hasara lakini cha kushangaza hawachukuliwi hatua zozote ilihali tunawafahamu.”
Hoja hiyo iliungwa mkono na Mhe. Rashid Nzelemela ambaye ni diwani wa Kata ya Ruaha Mbuyuni, ambapo alieleza jinsi uharibifu mkubwa unavyofanywa kwenye misitu na kuharibu uoto wa asili, nyara za serikali pamoja na wanyama mbalimbali.
“mapori yanachomwa na wahusika wapo wanaonekana katika maeneo yetu tunayoshinda lakini hatuoni hatua zozote zikichukuliwa dhidi yao, hii siyo sawa naomba wote wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.”
Aidha alitoa rai kwa mamlaka husika kuhakisha wanakua na utaratibu mzuri wa kuilinda misitu na
hiyo ni pamoja na kuwachukulia hatua kali kabisa kwa wale watakaobainika.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa