HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UFUGAJI NYUKI 2024/2025
UTANGULIZI
Ufugaji nyuki ni shughuli ya kufuga nyuki kwajili ya kupata mazao yatokanayo na nyuki kama vile asali,nta,maziwa ya malkia,sumu nyuki,gundi ya nyuki. Aidha ufugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo umesaidia kukuza kipato cha jamii kwa kuuza mazao yanapatikana kutokana na ufugaji nyuki. Zaidi ya kukuza kipato cha jamii ufugaji nyuki unasaidia katika utunzaji wa mazingira na uchavushaji wa mimea.
SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA
Katika kipindi cha miaka mitano (05) tumetekeleza mambo yafuatayo katika mambo ya ufugaji nyuki
KUUNDA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI
Katika kipindi cha miaka mitano 2020/21 hadi 2024/25 shughuli za uundaji wa vikundi vya ufugaji nyuki ilifanyika ambapo jumla ya vikundi 33 viliundwa vyenye idadi ya wanachama 828 na idadi ya mizinga 2063. Wafugaji walipewa vifaa kama mizinga na mavazi ili kuwasaidia katika shughuli za ufugaji nyuki.
Ifuatayo ni orodha ya wafugaji nyuki na idadi ya mizinga
| SN
|
JINA LA KIKUNDI/MFUGAJI/WAFUGAJI
|
SEHEMU (KIJIJI)
|
IDADI YA WANACHAMA/WAFUGAJI
|
IDADI YA MIZINGA
|
||
| 1
|
NEEMA
|
Makungu
|
32
|
100
|
||
| 2
|
UWANYUI
|
Ilula
|
30
|
150
|
||
| 3
|
CHAWANIKO
|
Ikokoto
|
30
|
20
|
|
|
| 4
|
KIWANYUKI
|
Kilolo
|
30
|
200
|
|
|
| 5
|
UHURU
|
Mkalanga
|
15
|
70
|
|
|
| 6
|
KIWANYUI
|
Ikokoto
|
20
|
40
|
|
|
| 7
|
MKOMBOZI
|
Masalali
|
15
|
15
|
|
|
| 8
|
TAMTAM
|
Mgowelo
|
30
|
25
|
|
|
| 9
|
UPENDO
|
Msosa
|
31
|
30
|
|
|
| 10
|
TWILUMBA
|
Kimala
|
21
|
51
|
|
|
| 11
|
PAMBAZUKO
|
Kimala
|
20
|
41
|
|
|
| 12
|
UNYUMIKI
|
Kising’a
|
30
|
41
|
|
|
| 13
|
MWINOME
|
Isagwa
|
30
|
30
|
|
|
| 14
|
SELEBU
|
Ibumu
|
30
|
30
|
|
|
| 15
|
UPENDO
|
Ruahambuyuni
|
32
|
30
|
|
|
| 16
|
KISATA
|
Ibumu
|
30
|
15
|
|
|
| 17
|
MKWILA
|
Magana
|
30
|
24
|
|
|
| 18
|
TUSONGEMBELE
|
Mlafu
|
30
|
30
|
|
|
| 19
|
TUPENDANE
|
Kipaduka
|
30
|
15
|
|
|
| 20
|
CHAWANI
|
Ilambo
|
15
|
30
|
|
|
| 21
|
CHAWNIRI
|
Irindi
|
15
|
30
|
|
|
| 22
|
CHAWAMA
|
Mahenge
|
15
|
75
|
|
|
| 23
|
MUUNGANO
|
Wotalisoli
|
10
|
120
|
|
|
| 24
|
Acacia Group
|
Kitelewasi
|
5
|
400
|
|
|
| 25
|
Kikundi 2
|
Mwatasi
|
30
|
37
|
|
|
| 26
|
Vikundi 2
|
Mbawi
|
45
|
50
|
|
|
| 27
|
Vikundi
|
Ng’ingula
|
30
|
50
|
|
|
| 28
|
Kikundi 1
|
Nyawegete
|
15
|
37
|
|
|
| 29
|
Kikundi 1
|
Masisiwe
|
30
|
50
|
|
|
| 30
|
Umoja wa Wanawake Kilolo
|
Kilolo
|
30
|
30
|
|
|
| 31
|
Steven Ndenga – Kikundi
|
Utengule
|
15
|
25
|
|
|
| 32
|
Kikundi cha vijana Degula wuki
|
Ilambo
|
6
|
121
|
|
|
| 33
|
UMOJA
|
Ilambo
|
51
|
51
|
|
|
| JUMLA
|
828
|
2063
|
|
|||
|
|
|
|
|
|
|
|
KUTOA MAFUNZO KWA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI
Katika miaka mitano tumefanikiwa kutoa mafunzo ya ufugaji nyukia katika vikundi 33, vyenye idadi ya wanachama 828. Mafunzo yaliyotolewa ni kama vile uanzishaji wa manzuki, uvunanji wa kisasa wa mazao ya nyuki, uchakataji wa mazao ya nyuki na kuongeza thamani kwenye mazao ya nyuki kwa kutengeneza wine, mafuta,kutengeneza vifungashio vya kisasa.
TAKWIMU ZA ASALI NA NTA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO
| S/N
|
MWAKA
|
ASALI (tani)
|
NTA (tani)
|
| 1
|
2020/21
|
38.996
|
2.246
|
| 2
|
2021/22
|
30.915
|
2.157
|
| 3
|
2022/23
|
42.900
|
2.151
|
| 4
|
2023/24
|
46.917
|
2.172
|
| 5
|
2024/25
|
58.767
|
2.214
|
KUWATAFUTIA MASOKO YA MAZAO YA NYUKI WAFUGAJI
Wafugaji nyuki wanakabiliwa na changamoto ya uhakika wa masoko licha ya kuwa na bidhaa bora kama vile asali na nta. Halmashauri ya Wilaya ya Killolo kipindi cha miaka mitano (5) tumefanikiwa kuwatafutia masoko wafugaji nyuki na kuwakutanisha na wadau mbalimbali.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imefanikisha wafugaji nyuki kushiriki katika maonyesho yanayoadhimishwa kila tarehe 8 mwezi wa 8 (nane nane) ili kuonesha mchango wao katika maendeleo ya sekta ya nyuki na kukuza kipato cha wafugaji nyuki.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa