
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imeendesha mafunzo ya maandalizi ya Mpango na Bajeti na mafunzo ya mfumo wa FFARS uliyoboreshwa (e-FFARS) kwa Watendaji wa Kata 24 na Vijiji 110.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Idara ya Mipango na Uratibu kwa kushirikiana na kitengo cha Fedha na Uhasibu, yametolewa kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 26 – 27 Oktoba, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya kilolo na ukumbi wa shule ya Sekondari Ilula ambapo walifundishwa kuhusiana na mfumo wa FFARS ulioboreshwa na uandaaji wa Mpango na Bajeti.

Aidha akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Dkt. John Mwingira amewaasa washiriki kutilia maanani mafunzo hayo kwakua ni muhimu sana, kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kukamilisha kwa wakati Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Wakati huohuo Dkt. Mwingira aliwasisitizia washiriki wa mafunzo hayo kuwa na bajeti shirikishi kwa wananchi kwenye maeneo yao kwa kuzingatia vipaumbele ili shughuli zitakazotekelezwa zilete matokeo chanya kwa jamii yote kwa ujumla.

Katika mafunzo hayo Washiriki walipata nafasi ya kuelekezwa kuwa katika mfumo wa FFARS maboresho yamefanyika, na kushauriwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa kwa vitu vya msingi ili kuendana na mfumo huo.





Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa