
Uzinduzi wa utoaji mikopo ya asilimia kumi (10%) umefanyika Oktoba 24, 2025 katika ukumbi uliopo mji mdogo wa Ilula na kualika wadau mbalimbali kuja kushuhudia tukio hilo.

Mchakato wa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye Ulemavu katika halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, ulianza mwezi Septemba 2024 baada ya Serikali kutangaza rasmi kurejesha mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.

Halmashauri ya Wilaya ya kilolo imetoa mikopo yenye thamani ya Tshs. 1,074,650,946/= kwa vikundi 104, kati ya hivyo vikundi vya Wanawake ni 60 vyenye jumla ya Tshs. 641,098,646/=, Vijana vikundi 34 vyenye jumla ya Tshs. 403,463,500/= na watu wenye Ulemavu vikundi 10 vyenye jumla ya Tshs. 30,088,800/=. Jumla ya wanachi 532 wamenufaika na mikopo hiyo wakiwemo; Wanawake 330, Vijana (KE 72 na ME 118) na watu wenye Ulemavu 16 (KE 6 na ME 10).

Akiongea katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Estomin Kyando ambaye ndiye alikua mgeni rasmi katika tukio hilo amesema, “ mikopo hii mkaitumie vizuri kwa malengo mliojiwekea na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine wapate nafasi ya kuomba na wao.”

Aidha Mhe. Kyando amepongeza kamati ya mikopo kwani wamechakata vikundi kwa haki na kwa usawa, na kuwasihi viongozi wa halmashauri kuepuka kujiingiza katika mikopo hiyo.

Mhe. Kyando amewasisitizia wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 Oktoba, 2025 ili kupiga kura ya Rais, Wabunge na Madiwani.

Naye afisa maendeleo wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo amewaasa wanufaika wa mikopo hiyo kutumia vizuri ili wajiongezee kipato na kukidhi mahitaji yao muhimu ili ilete tija kwao, familia zao na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa