• Kero |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Kilolo District Council
Kilolo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo,Umwagiliaji na ushirika
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi,Maliasili na Mazingira
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu
      • Ufugaji
    • Afya
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Customers services agreement
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofis au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii

maendeleo ya jamii

MAENDELEO YA JAMII                                                                                                                               

Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara 10 na vitengo 7 vinavyojitegemea katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, na ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za Halmashauri. 

MUUNDO WA IDARA

Idara ina vitengo Vikuu sita ambavyo ni:

  • Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi - 1
  •  Dawati la uratibu na usajili wa Ngo's, CBO's na FBO's - 1
  • Dawati la kusimamia masuala mtambuka - 1
  • Dawati la maendeleo ya mtoto - 1
  • Dawati la maendeleo ya jinsia -1
  • Dawati la ushirikishwaji jamii - 1

 SHUGHULI  ZA IDARA. 

Maendeleo ya Jamii

  • Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
  • Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
  • Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
  • Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbali mbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
  • Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
  • Kueneza elimu ya Uraia mwema.
  • Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
  • Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
  • Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
  • Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
  • Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
  • Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
  • Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
  • Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.


Maendeleo ya Vijana

  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana.
  • Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya vijana.
  • Kuhamasisha vijana kufufua moyo wa kujitolea kwa ajili ya Maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
  • Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya uzazi na kujamiina kwa Vijana.
  • Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, ajira kwa vijana na elimu ya familia kwa kushirikiana na Vyama visivyo vya kiserikali.
  • Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu vijana.
  • Kuratibu shughuli za NGOs mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Vijana.
  • Kuandaa mpango wa kuboresha malezi ya vijana.
  • Kuhamasisha waajiri na wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa vijana katika maeneo mbalimbali.
  • Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo vijana ili kuwawezesha kujiajiri.
  • Kuandaa mipango ya kuhamasisha vijana ili kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiajiri.
  • Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
  • Kuandaa na kuratibu shughuli za matamasha ya vijana.
  • Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs na CBOs zinazofanywa ngazi ya Wilaya.
  • Kuratibu mafunzo ya  utoaji wa mbinu za kuwasaidia vijana kujikomboa na umaskini, ujinga, kupiga vita UKIMWI, madawa ya kulevya na kutetea usawa wa jinsia

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 September 24, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA June 30, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA WATUMISHI WA UMMA December 23, 2024
  • Waliochaguliwa kuhudhuria usaili wa "Oral" October 10, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • VIKUNDI 104 VYANUFAIKA NA MIKOPO YA BILIONI MOJA NA ZAIDI.

    October 24, 2025
  • SHIRIKISHO LA UHIFADHI WA MAZINGIRA ASILIA (IUCN) LAFIKA KILOLO

    October 07, 2025
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI 48 WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WAPEWA MAFUNZO, KILOLO

    August 04, 2025
  • DAS - AIPOKEA UCSAF KILOLO

    July 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Jinsi ya Kupata leseni ya Biashara kupitia simu ya Mkononi
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Tangazo la Ajira

Viungio vinavyohusiana

  • Public Service Management
  • Watumishi Portal
  • PO-RALG
  • National Examination Council
  • eGA
  • Mkoa wa Iringa
  • Mufindi DC
  • Iringa DC
  • Iringa MC

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya

    Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo

    Simu ya mezani: 0262968010

    Mobile:

    Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa