
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Dkt. John Mwingira mapema leo tarehe 7/10/2025, amepokea ugeni kutoka shirikisho la uhifadhi wa mazingira asilia duniani (IUCN) katika ukumbi mdogo uliopo ndani ya halmashauri.

Afisa programa kutoka IUCN Bi. Sharon Kishenyi akitoa utambulisho wa shirikisho hilo mbele ya mkurugenzi na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo, amesema shrikisho la IUCN imekuja kutambulisha mradi wa RESOLVE NbS (suluhisho) kwa ngazi ya halmashauri wakiongozana na mbia mmoja kutoka CARE.
Bi. Sharon amesema mradi huo wa Resolve NbS (Suluhisho) ni mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa njia asilia, ambapo kwa Wilaya ya Kilolo vijiji vinne(4) ambavyo ni Mlafu,Isagwa, Mkalanga na Wotalisoli vitanufaika na mpango huo.

kwa upande wake Ndg. Abdulaziz Mkwizu (afisa programa wa IUCN) akiwasilisha utekelezaji wa mradi, amesema mradi huo wa suluhisho utakua wa miaka mitatu (2025/2027) ambapo kwa sasa wameanza na mikoa miwili ya Morogoro na Iringa huku ikihusisha Wilaya tano ambazo ni Ifakara, Mlimba, Morogoro vijijini, Iringa vijijini na Kilolo.

Aidha Ndg. Abdulaziz ameelezea mradi huo utajikita zaidi katika shughuli mbalimbali baadhi zikiwemo, kuboresha mipango ya matumizi bora ya ardhi, kurejesha ikolojia za misitu, ardhi na mito zilizoharibiwa, uwezo ya mifumo ya jamii katika kuweka na kukopa(VSLA),kuhamasisha jamii juu ya kilimo mseto na bayonuai, kuboresha mifumo ya uuzaji wa mazao kwa kutumia vyama vya ushirika(AMCOS) n.k.

Wakati huohuo amesisitiza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha ustahimilivu wa watu na rasilimali dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia masuluhisho asilia, na utekelezaji wa miradi hio ili iweze kufanikiwa zaidi watashirikiana na wabia wengine kutoka CARE, WWF, EAMCEF, CAN na CEOrT.

Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa