Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Jimbo la Kilolo wameanza kupata mafunzo ya siku tatu kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akifungua mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilolo Bi. Kemilembe Kafanabo amewaasa washiriki wa mafunzo hayo kusoma vizuri na kuzielewa sheria, katiba, kanuni na miongozo mbalimbali pamoja na maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na Tume.
“hakikisheni mnakua wazalendo katika hii kazi, jitahidini sana kuyaelewa majukumu yenu vizuri kwa kusoma sheria, katiba, kanuni na miongozo mbalimbali itakayokua inatolewa na Tume ili muwe na mpangilio mzuri ambao utasaidia kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa haki, utulivu na amani.” Amesema Kemilembe
Mafunzo hayo yamejumuisha washiriki 48 kutoka kata zote 24 za Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, ambapo kwa siku ya kwanza jumla ya mada 4 zimewasilishwa ambazo ni; majukumu ya watendaji wa uchaguzi, maadili na kampeni za uchaguzi,wajibu na majukumu ya watendaji wa vituo na utambulisho wa mawakala wa vyama vya siasa na uteuzi wa wagombea
Uchaguzi Mkuu wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo zaidi ya watu Milioni 30 waliojiandikisha wanatarajiwa kupiga kura siku hiyo.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa