Wataalamu kutoka Agriculture Transformation Office (ATO) iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, leo tarehe 19-12-2024 wametoa elimu na mafunzo kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuhusu Agriculture Master Plan 2050 – Mpango Mkuu wa Taifa wa Kilimo ambao lengo lake kuu ni kubainisha maeneo muhimu ya kilimo kama taifa.
Kaimu mkurugenzi kutoka ofisi ya mageuzi ya kilimo Ndugu Jeremiah Temi amewaomba wataalamu wakati wa kuandaa bajeti zao waweze pia kutenga bajeti za kilimo katika idara/vitengo vyao kulingana na muongozo wa mageuzi ya kilimo 2050, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kufikia lengo lililokusudiwa. Pia amesisitiza wataalamu wa kilimo wawe karibu na wakulima kwa kutoa ushauri kulingana na taratibu za kilimo zinavyotaka.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa