Jumuiya ya Tawala za Mitaa Iringa (ALAT) imefanya ziara katika halmashauri ya wilaya ya kilolo tarehe 18-12-2024 na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kusimamiwa na kutekelezwa ndani ya halmashauri.
Lengo kuu la jumuiya hii ni kukagua, kushauri na kuhimiza miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa inajengwa kwa ubora wa hali ya juu kulingana na thamani ya pesa iliyotolewa na inakamilishwa kwa wakati ili wananchi waweze kufurahia huduma za miradi hiyo.
Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada alipopata nafasi ya kuzungumza, amepongeza kwa usimamizi na kazi kubwa iliyofanyika katika miradi yote waliyopita,kwani miundombinu yake iliyowekwa imekaa vizuri na vifaa tiba vya kisasa vilivyopo katika hospitali ya wilaya ya kilolo ni vya hali ya juu sana.
“kwakweli tumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi za miradi ya maendeleo hapa kilolo, kwani hospitalini pale nimeona vifaa tiba vya kisasa kabisa na haya ni mapinduzi makubwa sana kwa wilaya na mkoa wetu kiujumla. Nawapongeza sana kwa uzalendo mliouonyesha wa kusimamia vizuri fedha za wananchi kutumika kwenye miradi kwa ukamilifu.” Alisema Ngwada
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa