Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Ggazi ya Wila kimefanyika tarehe 17-12-2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kikiongozwa na kaimu mwenyekiti, Katibu Tawala (W) Ndugu Estomin Kyando.
Katika kikao hicho kaimu mwenyekiti alitoa maagizo kwa wasimamizi kufwatilia na kuhakikisha mpango wa utoaji chakula shuleni unaimarishwa na watoto wote wawe wanapata chakula, pia alisisitiza hamasa zaidi itolewe kwa wanaume wawe na mazoea ya kuhudhuria katika matukio ya Afya na Lishe . pamoja na maagizo hayo alisisitiza elimu izidi kutolewa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Afua za lishe na ufuatiliaji wa watoto watakaozaliwa na kubainika na changamoto mbalimbali za kilishe.
“tujitahidi sana mpango wa kula mashuleni uwe endelevu na uzidi kuimarishwa zaidi ili kila mwanafunzi awe anapata chakula shuleni bila kukosa na hii itasaidia mtoto kusoma vizuri na kuelewa haraka darasani. Hatutaki watoto wetu wawe na udumavu wakati Iringa ni Mkoa unaozalisha vyakula mbalimbali kwa wingi nchini.” Alisema Kyando
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Ndugu Hassan Mnyikah alipopata nafasi ya kuzungumza alimshukuru kaimu mwenyekiti kwa maelekezo yote aliyoyatoa na kumuhakikishia atayatekeleza yote kwa wakati.
Akiendele kuzungumza Mnyikah aliwataka watendaji wote wahakikishe chakula kinachotolewa shuleni kiwe bora na salama na wanafunzi wote wanapata chakula. Pia alitoa agizo kwa watendaji hao ambao wana shule hazilishi chakula wanafunzi kutokana na sintofahamu kati ya kamati za chakula shuleni na walimu wakuu, waitishe mkutano wakae pamoja na waweke mazingira mazuri ya kuhakikisha chakula kinatolewa kwa wanafunzi wote, na mpaka tarehe 30-12-2024 awe ameshapata mrejesho kwa yale yote waliyokubaliana na kuamua.
“watendaji tukimaliza kikao hapa mkaitishe mkutano wa kamati za chakula shuleni pamoja na wakuu wa shule ili kwa pamoja mtengeneze mazingira mazuri ya wanafunzi kupata chakula wakiwa mashuleni na nawapa mpaka tarehe 30 mwezi huu muwe mshaniletea mrejesho ofisini kwangu.” Alisema Mnyikah
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa