Chuo cha serikali za mitaa chatoa mafunzo elekezi kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa mamlaka za serikali za mitaa na vijiji, kwa uongozi mpya uliochaguliwa tarehe 27-11-2024. Mafunzo haya yalitolewa kwa watendaji wa kijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa wilaya ya kilolo na mji mdogo wa ilula ambapo yalifanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 13 – 14/01/2025.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo ya kuzifahamu na kuzitambua sheria mbalimbali zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yao ya kilasiku yakutoa huduma kwa wananchi waliowachagua ili kuhakikisha haki na usawa kwa wote unatolewa, pia mada ya uongozi na utawala bora ilitolewa kwa viongozi hao wapate kufahamu kiongozi bora awe anasifa zipi na faida zake ni zipi.
Mafunzo haya elekezi yanalenga kuwawezesha washiriki kupata uelewa wa sheria zinazohusu uendeshaji wa hughuli za serikali za mitaa na vijiji nchini na dhana zima ya uongozi na utawala bora, ili waweze kuwaongoza wananchi wao kwa haki na usawa na kusukuma maendeleo kwa kasi kwa pamoja.
Chuo cha serikali za mitaa kimewawezesha kupata ufahamu na elimu ya pamoja kuzifahamu na kuzifuata sheria hususani pale wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwatumikia wananchi waliowachagua.
Wawezeshaji wa mafunzo haya yalitolewa na Ndugu Jonas Kapwani na Boniphace Kumburu kutoka chuo cha serikaliza mitaa.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa