Kuelekea zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, watendaji ngazi ya jimbo wamepatiwa mafunzo ya uboreshaji wa daftari kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 19 – 20/12/2024 yaliyofanyika ukumbi wa halmashauri ya wilaya kilolo.
Akifunga mafunzo hayo Ndugu Amelye Mfugale amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwani wanajukumu la kuwafundisha waandikishaji wasaidizi pamoja na waendesha mashine za bayometriki huku akiwasisitiza ushirikiano na utunzaji wa vifaa walivyopewa kufanyia kazi.
“tafadhalini sana hii ni kazi ya kitaifa hivyo naomba hili zoezi lifanyike kwa uweledi mkubwa, mshirikiane na maafisa kutoka tume pale ambapo mtaona kuna changamoto ili mpate kuuliza na wao hawatasita kuwasaidia.” Amesema Mfugale
Mafunzo hayo ya siku mbili yalitolewa ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo mada ya fomu Na. 1.5A, 5B na 2, mada ya fomu Na. 3A, 3B, 4, 6 NA 7 na mafunzo ya mfumo wa uandikishaji mada ambazo zilitanguliwa na kiapo kwa washiriki wote kuapa mbele ya hakimu.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa