Mwenge wa uhuru wa mwaka 2025 umeridhia miradi yote 11 ya halmashauri ya wilaya ya kilolo yenye thamani ya Tshs. Billion 1.6
Akizungumza na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Ismail Alli Ussi amesema ameridhishwa na miradi hiyo ambayo imetekelezwa kwa ubora na kuwa itakwenda kutumikia wananchi.
Aidha amewaomba wananchi kuitunza miradi hiyo kwani serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi wake.
Wakati huo huo amesisitiza elimu ya mpiga kura izidi kutolewa kwa wananchi ili wapate uelewa wa namna bora ya kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu na mapambano dhidi ya rushwa na matumizi ya nishati safi.
Kwa namna ya kipekee kabisa Ndg. Ismail ametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Rebecca Nsemwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bi. Siwema Jumaa kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuhakikisha miradi yote inasimamiwa vizuri na kumalizika kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha.
Ikumbukwe mwenge wa uhuru 2025, umepokelewa toka halmashauri ya Iringa dc tarehe 29/04/2025 katika viwanja vya Shule ya msingi Lundamatwe na kisha tarehe 30/04/2025 ukakabidhiwa Manispaa ya Iringa katika viwanja vya shule ya msingi Tagamenda.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa