Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe. Anna Msola amewaagiza wataalamu kutoka idara ya Ardhi kuongeza kasi ya kufuatilia majengo yote yanayojengwa kama yanavibali vya ujenzi, kwani kufanya hivyo itaondoa ujenzi holela wa makazi lakini kubwa zaidi halmashauri itakusanya mapato.
“watu wa ardhi tukipita maeneo mbalimbali ya wilaya yetu tunaona watu wanavyojenga majumba kwa kasi, lakini cha kushangaza wengi wao hawana vibali vya ujenzi hivyo nawamba anzisheni operesheni maalumu ya kukagua majengo yote yanayojengwa mhakikishe kama yana vibali na hii itatuongezea mapato lakini pia watu watajenga kwa kufuata ramani na hivyo kuupendezesha mji wetu.” Alisema Anna Msola
Aidha kwa upande wa wajumbe wa kamati hio wao walisisitizia swala zima la upungufu wa madawati na viti mashuleni na kushauri mikakati yote iliyopendekezwa na kupitishwa ili kuondokana na tatizo hilo ianze kutekelezwa mara moja ili ifikapo Januari watoto wote mashuleni wakae kwenye madawati na kwa nafasi.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ndugu Hassan Mnyikah aliishukuru kamati hio kwa maono na ushauri wao mzuri walioutoa na kuahidi kuufanyia kazi kwa vitendo ili kuhakikisha maendeleo ya halmshauri na ukusanyaji wa mapato unazidi kushamiri.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo tarehe 18-12-2024.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa