Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe.Rebecca Sanga Nsemwa ambaye pia ndie Mwenyekiti wa baraza la biashara, ameutangazia umma kuhusana na ujio wa maonyesho makubwa ya biashara, viwanda na kilimo yatakayofanyika tarehe 21-05-2025 katika viwanja vya Chuo cha Maendeleo FDC kilichopo mji mdogo wa Ilula.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo TCCIA, yakilenga kuwapatia nafasi wawekezaji, wafanyabiashara na wafugaji kuziona na kuzitambua fursa zilizopo Wilayani Kilolo ili wapate kuongeza na kutanua wigo wa uzalishaji, uwekezaji pamoja na masoko yao kiujumla.
Akizungumza katika kikao hicho cha Majadiliano ya Maonyesho hayo Rebecca Nsemwa amewaalika Wananchi wa Mkoa wa Iringa na maeneo ya jirani kuja kushiriki kikamilifu katika maonyesho hayo kwani yanatija kubwa sana kwa makundi mbalimbali yatakayoshiriki.
“Maonyesho hayo ni muhimu sana katika kukuza uchumi wetu wa wananchi wa Wilaya ya Kilolo na Mkoa wa Iringa kiujumla, kwani maonyesho yatajumuisha makampuni mbalimbali yatakayo onyesha jinsi ya kuongeza thamani katika mazao yetu pia wadau mbalimbali wa usindikaji na uwekezaji watashiriki.”
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na kilimo TCCIA Wilaya ya Kilolo, Charles Chavala ameeleza kuwa wamejipanga ipasavyo kufanikisha kwa ufanisi mkubwa maonyesho hayo, huku wakiamini kuwa wakazi wa wilaya ya kilolo watanufaika na maonyesho hayo kwa sekta zote zikiwemo kilimo, biashara ufugaji, viwanda n.k.
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa